Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Yoshua 22:6 - Swahili Revised Union Version Basi Yoshua akawabariki, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yoshua akawabariki na kuwaruhusu waende zao akawaambia, Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yoshua akawabariki na kuwaruhusu waende zao akawaambia, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yoshua akawabariki na kuwaruhusu waende zao akawaambia, Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani kwao. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao. BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akawabariki, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao. |
Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabariki watu kwa jina la BWANA wa majeshi.
Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake.
Ndipo Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake. Na Mikali, binti Sauli, akatoka nje aende kumlaki Daudi, naye akasema, Mfalme wa Israeli alikuwa mtukufu leo namna gani, akijifunua mwili wake mbele ya vijakazi vya watumishi wake, mfano wa watu baradhuli mmojawapo, ajifunuavyo mwili wake mbele ya watu, asipokuwa na haya!
Hata siku ya nane akaagana na watu, nao wakambarikia mfalme, wakaenda hemani kwao, wakifurahi na kuchangamka moyoni kwa wema wote BWANA aliomfanyia Daudi mtumishi wake, na Israeli watu wake.
Kwani wingi wa watu, naam, wengi wa Efraimu, na wa Manase, na wa Isakari, na wa Zabuloni, hawakujisafisha, lakini wakala Pasaka, ila si kama ilivyoandikwa. Naye Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, BWANA mwema na amsamehe kila mtu,
Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.
Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
Kisha Samweli aliwaambia watu kazi ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za BWANA. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake.
Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.
Naye Eli akambariki Elkana na mkewe, akasema, BWANA na akupe uzao kwa mwanamke huyu, wachukue mahali pa yule aliyemtoa kwa BWANA. Kisha wakarudi nyumbani kwao.