Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 22:7 - Swahili Revised Union Version

7 Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila la Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowaruhusu waende zao mahemani kwao, akawabariki,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7-8 “Rudini makwenu na utajiri mwingi; ng'ombe wenu wote, fedha, dhahabu, shaba, chuma na mavazi mengi. Gawaneni na ndugu zenu nyara zote mlizoziteka kutoka kwa maadui zenu.” Mose alikuwa ameyapa nusu ya kabila la Manase sehemu yao huko Bashani. Naye Yoshua akaipatia nusu ya pili ya kabila hilo sehemu yao huko magharibi ya mto Yordani kama alivyoyapa makabila yale mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Neno: Bibilia Takatifu

7 (Kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi mwa Yordani pamoja na ndugu zao.) Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 (Kwa nusu ya kabila la Manase Musa alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao). Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila la Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowaruhusu waende zao mahemani kwao, akawabariki,

Tazama sura Nakili

Yoshua 22:7
4 Marejeleo ya Msalaba  

Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.

Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo