Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 22:8 - Swahili Revised Union Version

8 kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Neno: Bibilia Takatifu

8 akisema, “Rudini nyumbani kwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia mavazi mengi; nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 akisema, “Rudini nyumbani mwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia wingi wa nguo, nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.

Tazama sura Nakili




Yoshua 22:8
12 Marejeleo ya Msalaba  

na upande wa mashariki akakaa hadi mwanzoni mwa jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe wao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.


Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na watu wote wa Yuda; basi akawa na mali na heshima tele.


Naye Hezekia akawa na mali nyingi mno na heshima; akajitengenezea hazina za fedha, za dhahabu, za vito, za manukato, za ngao, na za namna zote za vyombo vya thamani;


Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia; Na mwanamke akaaye nyumbani anagawa nyara.


Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.


ukagawanye nyara katika mafungu mawili; kati ya wanajeshi waliotoka nje kupigana vita na hio jumuiya nzima;


Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.


Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.


Tena ni nani atakayewasikiliza ninyi katika jambo hili? Kwa kuwa kama lilivyo fungu lake yeye ashukaye vitani, ndivyo litakavyokuwa na fungu lake huyo akaaye karibu na vyombo; watagawiwa sawasawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo