Ndivyo alivyotenda Daudi, vile vile kama BWANA alivyomwagiza; naye akawapiga Wafilisti toka Geba hata ujapo Gezeri.
Yoshua 18:24 - Swahili Revised Union Version na Kefar-amoni, na Ofni, na Geba; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kefar-amoni, Ofni na Geba. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema - BHND Kefar-amoni, Ofni na Geba. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kefar-amoni, Ofni na Geba. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Neno: Bibilia Takatifu Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake. Neno: Maandiko Matakatifu Kefar-Amoni, Ofni, na Geba; miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. BIBLIA KISWAHILI na Kefar-amoni, na Ofni, na Geba; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake; |
Ndivyo alivyotenda Daudi, vile vile kama BWANA alivyomwagiza; naye akawapiga Wafilisti toka Geba hata ujapo Gezeri.
Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu, makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, mtawala wa mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji.
wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.
Tena katika kabila la Benyamini, Gibeoni pamoja na mbuga zake za malisho, na Geba pamoja na mbuga zake za malisho;
Yonathani akaipiga hiyo ngome ya Wafilisti, iliyokuwako huko Gibea, nao Wafilisti wakapata habari. Naye Sauli akapiga tarumbeta katika nchi yote, huku akisema, Na wasikie Waebrania.