Ezra 2 - Swahili Revised Union VersionWatu waliorudi kutoka uhamishoni 1 Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; 2 ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya watu wa Israeli; 3 wazawa wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili. 4 Wazawa wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili. 5 Wazawa wa Ara, mia saba sabini na watano. 6 Wazawa wa Pahath-Moabu, wazawa wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wawili. 7 Wazawa wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. 8 Wazawa wa Zatu, mia tisa arubaini na watano. 9 Wazawa wa Zakai, mia saba na sitini. 10 Wazawa wa Binui, mia sita arubaini na wawili. 11 Wazawa wa Bebai, mia sita ishirini na watatu. 12 Wazawa wa Azgadi, elfu moja mia mbili ishirini na wawili. 13 Wazawa wa Adonikamu, mia sita sitini na sita. 14 Wazawa wa Bigwai, elfu mbili hamsini na sita. 15 Wazawa wa Adini, mia nne hamsini na wanne. 16 Wazawa wa Ateri, wazawa wa Hezekia, tisini na wanane. 17 Wazawa wa Besai, mia tatu ishirini na watatu. 18 Wazawa wa Harifu, mia moja na kumi na wawili. 19 Wazawa wa Hashumu, mia mbili ishirini na watatu. 20 Watu wa Gibari, tisini na watano. 21 Watu wa Bethlehemu, mia moja ishirini na watatu. 22 Watu wa Netofa, hamsini na sita. 23 Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane. 24 Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili. 25 Watu wa Kiriath-yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu. 26 Watu wa Rama na Geba, mia sita ishirini na mmoja. 27 Watu wa Mikmashi, mia moja ishirini na wawili. 28 Watu wa Betheli, na Ai, mia mbili ishirini na watatu. 29 Watu wa Nebo, hamsini na wawili. 30 Watu wa Magbishi, mia moja hamsini na sita. 31 Watu wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne. 32 Watu wa Harimu, mia tatu na ishirini. 33 Watu wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na watano. 34 Watu wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano. 35 Watu wa Senaa, elfu tatu mia sita na thelathini. 36 Makuhani; wazawa wa Yedaya, wa ukoo wa Yeshua, mia tisa sabini na watatu. 37 Wazawa wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili. 38 Wazawa wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba. 39 Wazawa wa Harimu, elfu moja na kumi na saba. 40 Walawi; wazawa wa Yeshua, wazawa wa Kadmieli wa wawazawa wa Hodavia, sabini na wanne. 41 Waimbaji; wazawa wa Asafu, mia moja ishirini na wanane. 42 Akina bawabu; wazawa wa Shalumu, wazawa wa Ateri, wazawa wa Talmoni, wazawa wa Akubu, wazawa wa Hatita, wazawa wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa. 43 Wanethini; wazawa wa Siha, wazawa wa Hasufa, wazawa wa Tabaothi; 44 wazawa wa Kerosi, wazawa wa Siaha, wazawa wa Padoni; 45 wazawa wa Lebana, wazawa wa Hagaba, wazawa wa Akubu; 46 wazawa wa Hagabu, wazawa wa Salmai, wazawa wa Hanani; 47 wazawa wa Gideli, wazawa wa Gahari, wazawa wa Reaya; 48 wazawa wa Resini, wazawa wa Nekoda, wazawa wa Gazamu; 49 wazawa wa Uza, wazawa wa Pasea, wazawa wa Besai; 50 wazawa wa Asna, wazawa wa Meunimu, wazawa wa Nefusimu; 51 wazawa wa Bakbuki, wazawa wa Hakufa, wazawa wa Harhuri; 52 wazawa wa Basluthi, wazawa wa Mehida, wazawa wa Harsha; 53 wazawa wa Barkosi, wazawa wa Sisera, wazawa wa Tema; 54 wazawa wa Nesia, wazawa wa Hatifa. 55 Wazawa wa watumishi wa Sulemani; wazawa wa Sotai, wazawa wa Soferethi, wazawa wa Peruda; 56 wazawa wa Yaala, wazawa wa Darkoni, wazawa wa Gideli; 57 wazawa wa Shefatia, wazawa wa Hatili, wazawa wa Pokereth-Sebaimu, wazawa wa Amoni. 58 Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili. 59 Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha koo za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli; 60 wazawa wa Delaya, wazawa wa Tobia na wazawa wa Nekoda, mia sita hamsini na wawili. 61 Tena wa makuhani; wazawa wa Habaya, wazawa wa Hakosi, wazawa wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. 62 Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. 63 Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu. 64 Basi hilo kusanyiko lote nzima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili na mia tatu na sitini, 65 tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili. 66 Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu wao, mia mbili arubaini na watano; 67 ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini. 68 Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake; 69 wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu sitini na moja, na mane za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani. 70 Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya