Ezra 2:1 - Swahili Revised Union Version1 Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema1 Wafuatao ni watu wa mkoani waliotoka utumwani ambao Nebukadneza mfalme wa Babuloni aliwapeleka mateka Babuloni, wakarudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda. Kila mtu alirudi mjini kwake. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND1 Wafuatao ni watu wa mkoani waliotoka utumwani ambao Nebukadneza mfalme wa Babuloni aliwapeleka mateka Babuloni, wakarudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda. Kila mtu alirudi mjini kwake. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza1 Wafuatao ni watu wa mkoani waliotoka utumwani ambao Nebukadneza mfalme wa Babuloni aliwapeleka mateka Babuloni, wakarudi mjini Yerusalemu na nchini Yuda. Kila mtu alirudi mjini kwake. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, Tazama suraBIBLIA KISWAHILI1 Basi hawa ndio watu wa mkoa, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka mpaka Babeli, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake; Tazama sura |
Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo dume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mabeberu kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na wakuu wa tarafa na wakuu wa mikoa kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi, mikoa mia moja na ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.