Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Yoshua 15:1 - Swahili Revised Union Version Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini. Biblia Habari Njema - BHND Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Eneo la nchi waliyopewa kwa kura watu wa kabila la Yuda kulingana na jamaa zake lilienea tangu kusini-mashariki hadi mpakani mwa Edomu. Sehemu ya kusini kabisa ilikuwa jangwa la Sini. Neno: Bibilia Takatifu Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea kufuatana na koo zao, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini. Neno: Maandiko Matakatifu Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini. BIBLIA KISWAHILI Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini. |
Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Basi, wakati ule Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, kutoka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, mbele za BWANA, Mungu wetu, siku saba na siku saba, yaani siku kumi na nne.
Na upande wa kusini, kuelekea kusini, utakuwa ni kutoka Tamari mpaka maji ya Meriba-Kadeshi, mpaka kijito cha Misri, mpaka bahari kubwa. Huu ndio upande wa kusini, kuelekea kusini.
Na mpakani mwa Reubeni, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Yuda, fungu moja.
tena tulipomlilia BWANA, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwa nchi yako;
na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.
kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli.
kwa kufuata hiyo kura ya urithi wao, vile vile kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, kwa ajili ya hayo makabila tisa, na hiyo nusu ya kabila.
Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini;
Watu hao wataigawanya nchi iwe mafungu saba; Yuda atakaa katika mpaka wake huko upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu watakaa katika mpaka wao upande wa kaskazini.