Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 14:2 - Swahili Revised Union Version

2 kwa kufuata hiyo kura ya urithi wao, vile vile kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, kwa ajili ya hayo makabila tisa, na hiyo nusu ya kabila.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Sehemu yao hiyo waligawiwa kwa kura kama vile Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose awape yale makabila tisa na nusu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Sehemu yao hiyo waligawiwa kwa kura kama vile Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose awape yale makabila tisa na nusu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Sehemu yao hiyo waligawiwa kwa kura kama vile Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose awape yale makabila tisa na nusu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Urithi wao uligawanywa kwa kura kwa yale makabila tisa na nusu, kama bwana alivyoamuru Musa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 kwa kufuata hiyo kura ya urithi wao, vile vile kama BWANA alivyoamuru kwa mkono wa Musa, kwa ajili ya hayo makabila tisa, na hiyo nusu ya kabila.

Tazama sura Nakili




Yoshua 14:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.


Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.


Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo.


Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;


Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.


Kisha Mfalme atawaambia wale walioko katika mkono wake wa kulia, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;


Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.


Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila tisa, na nusu ya kabila la Manase.


Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.


Nanyi mtaiandika nchi iwe mafungu saba, kisha hayo maandiko yake mtaniletea mimi hapa; nami nitawapigia kura hapa mbele ya BWANA, Mungu wetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo