Yohana 7:24 - Swahili Revised Union Version Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki.” Biblia Habari Njema - BHND Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki.” Neno: Bibilia Takatifu Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.” Neno: Maandiko Matakatifu Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.” BIBLIA KISWAHILI Basi msihukumu kwa kuangalia kwa nje tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. |
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
BWANA wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;
Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo ndivyo sisi nasi tulivyo.
Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.