Yohana 11:24 - Swahili Revised Union Version Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Biblia Habari Njema - BHND Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Neno: Bibilia Takatifu Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.” Neno: Maandiko Matakatifu Martha akamjibu, “Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho.” BIBLIA KISWAHILI Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. |
Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.
nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Na mapenzi yake aliyenituma ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.
Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Nina tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.
Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;