Yoeli 1:12 - Swahili Revised Union Version Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imetoweka kwa wanadamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu. Biblia Habari Njema - BHND Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mizabibu imenyauka; mitini imedhoofika; mikomamanga, mitende na mitofaa imekauka, naam miti yote shambani imekauka. Furaha imetoweka miongoni mwa watu. Neno: Bibilia Takatifu Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka. Neno: Maandiko Matakatifu Mzabibu umekauka na mtini umenyauka; mkomamanga, mtende na mtofaa, miti yote shambani, imekauka. Hakika furaha yote ya mwanadamu imeondoka. BIBLIA KISWAHILI Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imetoweka kwa wanadamu. |
Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Niliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake niliyaonja kuwa matamu.
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Pana kilio katika njia kuu kwa sababu ya divai; furaha yote imetiwa giza, na changamko la nchi limetoweka.
Umeliongeza taifa, umezidisha furaha yao; Wanafurahi mbele zako, Kama furaha ya wakati wa mavuno, Kama watu wafurahivyo wagawanyapo nyara.
Furaha na shangwe zimeondoshwa, katika shamba lizaalo sana, na katika nchi ya Moabu; nami nimeikomesha divai katika mashinikizo; hapana mtu atakayekanyaga zabibu kwa shangwe; shangwe ile itakuwa si shangwe.
Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?
Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akatayarisha buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakatika.
Je, Mbegu ingali ghalani? Naam, huo mzabibu, wala mtini, wala mkomamanga, wala mzeituni, haikuzaa kitu; tangu siku hii ya leo nitawabariki.
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.
Wakafika bonde la Eshkoli, na huko wakakata tawi lenye kishada kimoja cha zabibu, wakalichukua kwa mti kati ya watu wawili; wakaleta makomamanga pia, na tini.