ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Yakobo 4:10 - Swahili Revised Union Version Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. Biblia Habari Njema - BHND Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. Neno: Bibilia Takatifu Jinyenyekezeni mbele za Mwenyezi Mungu, naye atawainua. Neno: Maandiko Matakatifu Jinyenyekezeni mbele za Mwenyezi Mungu, naye atawainua. BIBLIA KISWAHILI Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. |
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Bwana MUNGU asema hivi; Kiondoe kilemba, livue taji; haya hayatakuwa tena kama yalivyo; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;