Yakobo 2:23 - Swahili Revised Union Version Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.” Biblia Habari Njema - BHND Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.” Neno: Bibilia Takatifu Kwa njia hiyo likatimizwa andiko lisemalo, “Ibrahimu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Ibrahimu alimwamini Mwenyezi Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mwenyezi Mungu. BIBLIA KISWAHILI Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. |
na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme.
Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Abrahamu rafiki yako hata milele?
Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata kambini; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.
Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Na pamoja naye walisulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kulia na mmoja mkono wake wa kushoto. [
Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;
Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na Maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,
Kwa maana Maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nioneshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.