Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yakobo 2:23 - Swahili Revised Union Version

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: “Abrahamu alimwamini Mungu, na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Kwa njia hiyo likatimizwa andiko lisemalo, “Ibrahimu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Kwa njia hiyo yakatimizwa yale Maandiko yasemayo, “Ibrahimu alimwamini Mwenyezi Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki,” naye akaitwa rafiki wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Yakobo 2:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.


na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme.


Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Abrahamu rafiki yako hata milele?


Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu, Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.


Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata kambini; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.


Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Abrahamu, rafiki yangu;


Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Na pamoja naye walisulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kulia na mmoja mkono wake wa kushoto. [


Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.


Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;


Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na Maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,


Kwa maana Maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nioneshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


Kama vile Abrahamu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.


Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;


Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.


Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo