Waebrania 7:21 - Swahili Revised Union Version (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa, wala hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Biblia Habari Njema - BHND Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa, wala hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa, wala hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Neno: Bibilia Takatifu lakini Isa alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Mwenyezi Mungu ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Neno: Maandiko Matakatifu lakini Isa alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mwenyezi Mungu alimwambia: “bwana Mwenyezi ameapa naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’ ” BIBLIA KISWAHILI (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;) |
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?
Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.