Waebrania 10:35 - Swahili Revised Union Version Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. Biblia Habari Njema - BHND Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, msipoteze uhodari wenu, maana utawapatia tuzo kubwa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno. BIBLIA KISWAHILI Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. |
Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa angaa kikombe cha maji baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.
Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.