Nehemia 5:7 - Swahili Revised Union Version Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nikaamua kuchukua hatua. Nikawashutumu wakuu na maofisa, nikawaambia, “Mnawatoza riba ndugu zenu.” Biblia Habari Njema - BHND Nikaamua kuchukua hatua. Nikawashutumu wakuu na maofisa, nikawaambia, “Mnawatoza riba ndugu zenu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nikaamua kuchukua hatua. Nikawashutumu wakuu na maofisa, nikawaambia, “Mnawatoza riba ndugu zenu.” Neno: Bibilia Takatifu Nikayatafakari katika akili yangu, nikiwalaumu wakuu na maafisa. Nikawaambia, “Mnawaonea ndugu zenu kwa kuwatoza riba!” Basi nikaita mkutano mkubwa ili kukabiliana nao, Neno: Maandiko Matakatifu Nikayatafakari katika akili yangu, nikiwalaumu wakuu na maafisa. Nikawaambia, “Mnawaonea ndugu zenu kwa kuwatoza riba!” Basi nikaitisha mkutano mkubwa ili kuwashughulikia BIBLIA KISWAHILI Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao. |
BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu?
Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?
na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.
Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.
Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; acheni kutoza kwenu kwa nguvu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nilishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu.