Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
Nehemia 3:26 - Swahili Revised Union Version (basi Wanethini hukaa Ofeli), mpaka mahali paelekeapo lango la maji kukabili mashariki, nao mnara utokezao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akishirikiana na watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli, walijenga upya sehemu inayokabiliana na Lango la Maji, upande wa mashariki na mnara mrefu. Biblia Habari Njema - BHND akishirikiana na watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli, walijenga upya sehemu inayokabiliana na Lango la Maji, upande wa mashariki na mnara mrefu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akishirikiana na watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli, walijenga upya sehemu inayokabiliana na Lango la Maji, upande wa mashariki na mnara mrefu. Neno: Bibilia Takatifu na watumishi wa Hekalu walioishi juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki na ule mnara uliochomoza. Neno: Maandiko Matakatifu na watumishi wa Hekalu walioishi juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki na ule mnara uliojitokeza. BIBLIA KISWAHILI (basi Wanethini hukaa Ofeli), mpaka mahali paelekeapo lango la maji kukabili mashariki, nao mnara utokezao. |
Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana.
Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya Lango la Sameki; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka makamanda wa jeshi katika miji yote ya Yuda yenye maboma.
Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;
na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki.
Baada yake wakajenga Watekoi sehemu nyingine, kuuelekea mnara mkubwa utokezao, na mpaka ukuta wa Ofeli.
Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha Torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli.
Basi watu wote wakatoka, wakayaleta, wakajitengenezea vibanda, kila mtu juu ya dari la nyumba yake, na katika nyua zao, na katika nyua za nyumba ya Mungu, na katika uwanja wa lango la maji, na katika uwanja wa lango la Efraimu.
Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.
maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda mwitu, malisho ya makundi ya kondoo;