Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nehemia 8:3 - Swahili Revised Union Version

3 Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kisha watu wote wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuelewa, Ezra aliwasomea sheria ya Mose akiwa mbele ya Lango la Maji tangu asubuhi hadi adhuhuri. Watu wote wakatega masikio yao kusikiliza kwa makini kitabu cha sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko hadi adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Torati.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri, akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Torati.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.

Tazama sura Nakili




Nehemia 8:3
25 Marejeleo ya Msalaba  

wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;


Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;


Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha Torati ya Musa, BWANA aliyowaamuru Israeli.


Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hadi siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha Torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.


Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameitengeneza kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kulia; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu.


Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama;


Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na watu wengi walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.


wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.


Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.


Kisha, baada ya Torati na kitabu cha Manabii kusomwa, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.


Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.


Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.


Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa hamu kuu, wakayachunguza Maandiko kila siku, ili waone kama mambo hayo ndivyo yalivyo.


Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hadi alfajiri, ndipo akaenda zake.


Siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubia, maana aliazimia kusafiri siku iliyofuata, naye akafululiza maneno yake hadi usiku wa manane.


Wakiisha kupanga naye siku, wakamjia katika nyumba aliyokaa, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya Sheria ya Musa na ya manabii, tangu asubuhi hadi jioni.


Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli.


Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.


Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo