Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nehemia 8:2 - Swahili Revised Union Version

2 Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Ezra, ambaye alikuwa kuhani, akaenda na kukileta kitabu cha sheria ya Mose mbele ya mkutano mzima, wanaume kwa wanawake na yeyote aliyeweza kuielewa hiyo sheria aliposikia. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Torati mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Torati mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza ya mwezi wa saba.

Tazama sura Nakili

Nehemia 8:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;

Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;

Tena siku baada ya siku, tangu siku ya kwanza hadi siku ya mwisho, akasoma katika kitabu cha Torati ya Mungu. Wakafanya sikukuu muda wa siku saba; na siku ya nane palikuwa na kusanyiko la makini, kama ilivyoagizwa.

Naye Nehemia, ndiye aliyekuwa Tirshatha, na Ezra kuhani, mwandishi, na Walawi waliowafundisha watu, wakawaambia watu wote, Siku hii ni takatifu kwa BWANA, Mungu wenu; msiomboleze wala msilie. Maana watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati.

Hata siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wana wa Israeli wakawa wamekusanyika, wakifunga, wenye kuvaa magunia, na kujitia udongo vichwani.

Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini?

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu.

Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.

Tena mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi; ni siku ya kupiga tarumbeta kwenu.

Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.

Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika kitabu, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi;

Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo