Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nehemia 10:28 - Swahili Revised Union Version

28 Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Sisi sote watu wa Israeli, makuhani, Walawi, wangoja malango, waimbaji, watumishi wa hekalu na watu wote waliojitenga na mataifa jirani kufuata sheria ya Mungu pamoja na wake zao, wana wao na binti zao, wote wenye maarifa na fahamu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Sisi sote watu wa Israeli, makuhani, Walawi, wangoja malango, waimbaji, watumishi wa hekalu na watu wote waliojitenga na mataifa jirani kufuata sheria ya Mungu pamoja na wake zao, wana wao na binti zao, wote wenye maarifa na fahamu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Sisi sote watu wa Israeli, makuhani, Walawi, wangoja malango, waimbaji, watumishi wa hekalu na watu wote waliojitenga na mataifa jirani kufuata sheria ya Mungu pamoja na wake zao, wana wao na binti zao, wote wenye maarifa na fahamu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 “Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu, na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Torati ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao wote wa kiume na wa kike waliokuwa na uwezo wa kufahamu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 “Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu, na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Torati ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

28 Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;

Tazama sura Nakili

Nehemia 10:28
16 Marejeleo ya Msalaba  

Hivyo makuhani, na Walawi, na baadhi ya watu, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, wakakaa mijini mwao, naam, Israeli wote wakakaa mijini mwao.

Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka BWANA, Mungu wa Israeli,

Maluki, Harimu, na Baana.

Ikawa walipoisikia Torati, wakawatenga Israeli na umati wa watu waliochanganyika nao.

Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.

Waliokuwa wa wazao wa Israeli wakajitenga na wageni wote, wakasimama, wakaziungama dhambi zao, na maovu ya baba zao.

Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa zaburi.

Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.

nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.

Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni BWANA, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.

Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo