Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Nehemia 3:25 - Swahili Revised Union Version

25 Baada yake akajenga Palali, mwana wa Uzai, kuelekea ugeukapo ukuta, nao mnara utokezao penye nyumba ya juu ya kifalme, iliyopo karibu na uwanda wa walinzi. Baada yake akajenga Pedaya, mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Sehemu inayofuata, tokea pembeni mwa ukuta na mnara wa ikulu ya juu karibu na uwanda wa ulinzi ilijengwa upya na Palali, mwana wa Uzai. Pedaia, mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Sehemu inayofuata, tokea pembeni mwa ukuta na mnara wa ikulu ya juu karibu na uwanda wa ulinzi ilijengwa upya na Palali, mwana wa Uzai. Pedaia, mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Sehemu inayofuata, tokea pembeni mwa ukuta na mnara wa ikulu ya juu karibu na uwanda wa ulinzi ilijengwa upya na Palali, mwana wa Uzai. Pedaia, mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Naye Palali, mwana wa Uzai alijenga sehemu iliyokuwa mkabala na pembe ya ukuta, hadi kwenye mnara wa juu ambao unachomoka kuanzia kwenye jumba la kifalme, kando ya ua wa walinzi. Baada yake, Pedaya mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Naye Palali, mwana wa Uzai alijenga sehemu iliyokuwa mkabala na pembe ya ukuta, mpaka kwenye mnara wa juu ambao unajitokeza kuanzia kwenye jumba la kifalme, kando ya ua wa walinzi. Baada yake, Pedaya mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 Baada yake akajenga Palali, mwana wa Uzai, kuelekea ugeukapo ukuta, nao mnara utokezao penye nyumba ya juu ya kifalme, iliyopo karibu na uwanda wa walinzi. Baada yake akajenga Pedaya, mwana wa Paroshi,

Tazama sura Nakili

Nehemia 3:25
12 Marejeleo ya Msalaba  

wazawa wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.

na juu ya lango la Efraimu, na kupita lango la kale, na lango la samaki, na mnara wa Hananeli, na mnara wa Hamea, mpaka lango la kondoo; nao wakasimama hapo langoni pa gereza.

Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.

Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameitengeneza kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kulia; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu.

Asemaye, Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana; Naye hujikatia madirisha; Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi, Na kupakwa rangi nyekundu.

Basi, wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli liliuzunguka Yerusalemu; na Yeremia, nabii, alikuwa amefungwa ndani ya uwanja wa walinzi, uliokuwa katika nyumba ya mfalme wa Yuda.

Tena, neno la BWANA likamjia Yeremia mara ya pili, hapo alipokuwa angali amefungwa katika uwanja wa walinzi, kusema,

Ndipo Sedekia mfalme akatoa amri, wakamtia Yeremia katika ukumbi wa walinzi; wakampa kila siku mkate mmoja uliotoka katika njia ya waokaji, hata mkate wote wa mji ulipokwisha. Basi Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.

Basi wakamwinua Yeremia kwa kamba hizo, wakamtoa shimoni; naye Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.

Nao Wakaldayo wakaiteketeza nyumba ya mfalme, na nyumba za watu kwa moto, wakazibomoa kuta za Yerusalemu.

Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo