Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
Nehemia 13:23 - Swahili Revised Union Version Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena wakati huo niliona Wayahudi waliooa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu; Biblia Habari Njema - BHND Tena wakati huo niliona Wayahudi waliooa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena wakati huo niliona Wayahudi waliooa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu; Neno: Bibilia Takatifu Zaidi ya hayo, niliona Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu. Neno: Maandiko Matakatifu Zaidi ya hayo, niliona Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake kutoka Ashdodi, Amoni na Moabu. BIBLIA KISWAHILI Tena siku zizo hizo nikawaona wale Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, na Amoni, na Moabu; |
Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,
Kisha Ezra, kuhani, akasimama, akawaambia, Mmekosa, mmeoa wanawake wageni, kuiongeza hatia ya Israeli.
tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula chochote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena mwaka wa saba tusiliwe na madeni yote tuyafute.
Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;
na nusu ya watoto wao wakazungumza kwa lugha ya Ashdodi, wala hawakuweza kuzungumza Kiyahudi, bali kwa lugha mojawapo ya watu hao.
Basi, na sisi, je! Tuwasikilize ninyi kutenda neno hili baya, hata kumkosea Mungu wetu kwa kuwaoa wanawake wageni?
Lakini ikawa, Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;
Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
Nao wakaoa wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Baada ya kukakaa huko miaka kumi hivi,
Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Ebenezeri hadi Ashdodi.