Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nehemia 4:7 - Swahili Revised Union Version

7 Lakini ikawa, Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na Waashdodi waliposikia kuwa ujenzi mpya wa ukuta wa Yerusalemu ulikuwa unasonga mbele na kwamba mapengo katika ukuta yanazibwa barabara, wao walizidi kukasirika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na Waashdodi waliposikia kuwa ujenzi mpya wa ukuta wa Yerusalemu ulikuwa unasonga mbele na kwamba mapengo katika ukuta yanazibwa barabara, wao walizidi kukasirika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na Waashdodi waliposikia kuwa ujenzi mpya wa ukuta wa Yerusalemu ulikuwa unasonga mbele na kwamba mapengo katika ukuta yanazibwa barabara, wao walizidi kukasirika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini wakati Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na watu wa Ashdodi waliposikia kuwa ukarabati wa kuta za Yerusalemu ulikuwa umeendelea, na mianya ilikuwa inazibwa, walikasirika sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini wakati Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni na watu wa Ashdodi waliposikia kuwa ukarabati wa kuta za Yerusalemu ulikuwa umeendelea na mianya ilikuwa inazibwa, walikasirika sana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Lakini ikawa, Sanbalati, Tobia, Waarabu, Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;

Tazama sura Nakili




Nehemia 4:7
29 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.


Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.


Baada ya hayo, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani.


Na ajue mfalme ya kuwa sisi tuliingia nchi ya Yuda, tukafika kunako nyumba ya Mungu mkuu, iliyojengwa kwa mawe makubwa, na miti imetiwa katika kuta zake, na kazi hii inaendelea kwa bidii, na kusitawi katika mikono yao.


Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli.


Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?


Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akawa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.


Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaunganishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.


wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.


Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo wamataifa wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.


na watu wote waliochanganyika pamoja, na wafalme wote wa nchi ya Uzi, na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;


Kisha Ishmaeli akawachukua mateka watu wote waliosalia, waliokuwa huko Mizpa, yaani, binti za mfalme, na watu wote waliobaki Mizpa, ambao Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alikuwa amemkabidhi Gedalia, mwana wa Ahikamu; Ishmaeli, mwana wa Nethania, akawachukua mateka. Akaondoka, ili awaendee wana wa Amoni.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;


Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.


Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake.


Wao waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakapanga kuwaua.


Joka likamkasirikia yule mwanamke, likaenda zake lifanye vita juu ya wazawa wake waliobakia, wanaozishika amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; nalo likasimama juu ya mchanga wa bahari.


Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hili mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kulia; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo