Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 11:1 - Swahili Revised Union Version

1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Solomoni alipenda sana wanawake wa kigeni: Binti Farao, wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Solomoni alipenda sana wanawake wa kigeni: Binti Farao, wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Solomoni alipenda sana wanawake wa kigeni: binti Farao, wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mbali na binti Farao, Mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni: Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hata hivyo, Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 11:1
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.


Naye Rehoboamu mwana wa Sulemani akatawala katika Yuda. Rehoboamu akaanza kutawala alipokuwa mwenye miaka arubaini na mmoja, akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua BWANA miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke jina lake huko. Na jina la mamaye aliitwa Naama, Mwamoni.


Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na jina la mamaye aliitwa Naama, Mwamoni. Na mwanawe, Abiya, alitawala mahali pake.


Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.


Huyo Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi, hata alipokwisha kuijenga nyumba yake, na nyumba ya BWANA, na ukuta wa kuuzunguka Yerusalemu.


Hao wote walikuwa wameoa wanawake wageni; na wake zao wengine walikuwa wamezaa watoto.


Na mambo hayo yalipotendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, na machukizo yao, yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori.


Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na viongozi umetangulia katika kosa hili.


Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.


Ili kuokoka na malaya, Naam, malaya mwenye kubembeleza kwa maneno yake;


Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.


Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.


Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wanaowaharibu wafalme.


Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate, Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.


Wapate kukulinda na malaya, Na mwasherati akubembelezaye kwa maneno yake.


Wala usitwae mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai.


Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo