Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
Nahumu 2:8 - Swahili Revised Union Version Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ninewi ni kama bwawa lililobomoka, watu wake wanaukimbia ovyo. “Simameni! Simameni!” Sauti inaita, lakini hakuna anayerudi nyuma. Biblia Habari Njema - BHND Ninewi ni kama bwawa lililobomoka, watu wake wanaukimbia ovyo. “Simameni! Simameni!” Sauti inaita, lakini hakuna anayerudi nyuma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ninewi ni kama bwawa lililobomoka, watu wake wanaukimbia ovyo. “Simameni! Simameni!” sauti inaita, lakini hakuna anayerudi nyuma. Neno: Bibilia Takatifu Ninawi ni kama dimbwi, nayo maji yake yanakauka. Wanalia, “Simama! Simama!” Lakini hakuna anayegeuka nyuma. Neno: Maandiko Matakatifu Ninawi ni kama dimbwi, nayo maji yake yanakauka. Wanalia, “Simama! Simama!” Lakini hakuna anayegeuka nyuma. BIBLIA KISWAHILI Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma. |
Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe.
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wanajimu, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe kutoka kwa mambo yatakayokupata.
Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.
Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.
Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.
Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake.
Ewe ukaaye juu ya maji mengi, uliye na hazina nyingi, mwisho wako umewadia, kadiri ya tamaa zako.
Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana; Wanakaa katika ngome zao; Ushujaa wao umewapungukia; Wamekuwa kama wanawake; Makao yake yameteketea; Makomeo yake yamevunjika.
Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, wala hapana ajuaye walikokwenda.
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.