Nahumu 2:7 - Swahili Revised Union Version Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipigapiga vifua vyao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mji uko wazi kabisa, watu wamechukuliwa mateka. Wanawake wake wanaomboleza, wanalia kama njiwa, na kujipigapiga vifuani. Biblia Habari Njema - BHND Mji uko wazi kabisa, watu wamechukuliwa mateka. Wanawake wake wanaomboleza, wanalia kama njiwa, na kujipigapiga vifuani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mji uko wazi kabisa, watu wamechukuliwa mateka. Wanawake wake wanaomboleza, wanalia kama njiwa, na kujipigapiga vifuani. Neno: Bibilia Takatifu Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe na upelekwe uhamishoni. Vijakazi wake wanaomboleza kama hua na kupigapiga vifua vyao. Neno: Maandiko Matakatifu Imeagizwa kwamba mji uchukuliwe na upelekwe uhamishoni. Vijakazi wake wanaomboleza kama hua na kupigapiga vifua vyao. BIBLIA KISWAHILI Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipigapiga vifua vyao. |
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
Sisi sote twanguruma kama dubu; twaomboleza kama hua; twatazamia hukumu ya haki, lakini hapana; na wokovu, lakini u mbali nasi.
Lakini watakaokimbia watakimbia, nao watakuwa juu ya milima kama hua wa bondeni, wote wakilia, kila mmoja katika uovu wake.
Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako.
Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea.
Na makutano yote ya watu waliokuwa wamekutanika kutazama mambo hayo, walipoona yaliyotendeka, wakaenda zao kwao, wakijipigapiga vifua.