Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.
Mwanzo 21:9 - Swahili Revised Union Version Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Abrahamu, anafanya dhihaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baadaye Sara alimwona Ishmaeli, mtoto wa Abrahamu aliyezaliwa na Hagari, Mmisri, akicheza na Isaka mwanawe. Biblia Habari Njema - BHND Baadaye Sara alimwona Ishmaeli, mtoto wa Abrahamu aliyezaliwa na Hagari, Mmisri, akicheza na Isaka mwanawe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baadaye Sara alimwona Ishmaeli, mtoto wa Abrahamu aliyezaliwa na Hagari, Mmisri, akicheza na Isaka mwanawe. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hajiri Mmisri alimzalia Ibrahimu alikuwa anadhihaki. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Ibrahimu alikuwa anadhihaki, BIBLIA KISWAHILI Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Abrahamu, anafanya dhihaka. |
Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.
Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.
Kuhusu Ishmaeli nimekusikia, nimembariki na nitamzidisha na kumwongeza sana. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, na atakuwa na taifa kuu.
Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
Basi matarishi wakapita mji kwa mji kati ya nchi ya Efraimu na Manase, hata kufika Zabuloni; lakini waliwacheka na kuwadhihaki.
lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha, Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.
Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Siku za mateso na misiba yake, Yerusalemu huyakumbuka matamanio yake yote Yaliyokuwa tangu siku za kale; Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi, Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia; Hao watesi wake walimwona, Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Abrahamu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mwingine kwa mwanamke huru.
Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.
wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa minyororo, na kwa kutiwa gerezani;