Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 21:8 - Swahili Revised Union Version

8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Isaka akaendelea kukua, na siku alipoachishwa kunyonya, Abrahamu akafanya sherehe kubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Isaka akaendelea kukua, na siku alipoachishwa kunyonya, Abrahamu akafanya sherehe kubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Isaka akaendelea kukua, na siku alipoachishwa kunyonya, Abrahamu akafanya sherehe kubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya. Siku ile Isaka aliyoachishwa kunyonya, Ibrahimu alifanya sherehe kubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaka alipoachishwa kunyonya, Ibrahimu alifanya sherehe kubwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 21:8
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.


Akasema, Ni nani angemwambia Abrahamu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.


Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Abrahamu, anafanya dhihaka.


Basi akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa.


Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu.


Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.


Basi Abneri akamwendea Daudi huko Hebroni, akiwa na watu ishirini. Daudi akamfanyia karamu Abneri, na watu wote waliokuwa pamoja naye.


Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.


mwaka wa tatu wa kutawala kwake, ikawa aliwafanyia karamu wakuu na mawaziri wake; wakuu wa majeshi ya Uajemi na Umedi; watu maarufu na wakuu wa mikoa, wakihudhuria mbele zake.


Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya Kifuani mwa mama yake; Roho yangu ni kama mtoto, Aliyeachishwa kunyonya.


Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama kunyonya, akachukua mimba, akazaa mtoto wa kiume.


Basi babaye akamteremkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa ndivyo vijana walivyokuwa wakifanya.


Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mnaweza kunitegulia katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo nitakapowapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu;


Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa kunyonya, hapo ndipo nitakapomleta, ili awepo mbele za BWANA, akae huko daima.


Naye alipomwachisha kunyonya, akamchukua pamoja naye, na ng'ombe watatu, na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo.


Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hadi kulipopambazuka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo