Mika 5:9 - Swahili Revised Union Version Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli watawashinda adui zao na kuwaangamiza kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli watawashinda adui zao na kuwaangamiza kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu asema, “Wakati huo nitawaondoa farasi wenu, na kuyaharibu magari yenu ya farasi. Neno: Bibilia Takatifu Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, nao adui zako wote wataangamizwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako, nao adui zako wote wataangamizwa. BIBLIA KISWAHILI Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauawe mbali. |
nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;
Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.
BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.
Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.