Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mika 1:4 - Swahili Revised Union Version

Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Milima itayeyuka chini ya nyayo zake, kama nta karibu na moto; mabonde yatapasuka, kama maji yaporomokayo kwenye mteremko.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yanayotiririka kasi kwenye mteremko.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mika 1:4
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka; Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka.


Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.


Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA, Mbele za Bwana wa dunia yote.


Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Nili, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.


Milima hutetema mbele zake, navyo vilima huyeyuka; nayo dunia huinuliwa mbele za uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake.


Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.


Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.


Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.


Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.


BWANA, ulipotoka katika Seiri, Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu, Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondosha maji, Naam, mawingu yakadondosha maji.