Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 5:4 - Swahili Revised Union Version

4 BWANA, ulipotoka katika Seiri, Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu, Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondosha maji, Naam, mawingu yakadondosha maji.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 “Ee Mwenyezi-Mungu, ulipotoka huko Seiri, ulipoteremka mlimani Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu zilidondosha maji, naam, mawingu yakaiangusha mvua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 “Ee Mwenyezi-Mungu, ulipotoka huko Seiri, ulipoteremka mlimani Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu zilidondosha maji, naam, mawingu yakaiangusha mvua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 “Ee Mwenyezi-Mungu, ulipotoka huko Seiri, ulipoteremka mlimani Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu zilidondosha maji, naam, mawingu yakaiangusha mvua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 “Ee Mwenyezi Mungu, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “Ee bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 BWANA, ulipotoka katika Seiri, Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu, Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondosha maji, Naam, mawingu yakadondosha maji.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 5:4
13 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa,

Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasukasuka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.

Aitikisaye dunia itoke mahali pake, Na nguzo zake hutetemeka.

Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.

Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa.

Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;

Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.

Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.

Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.

ambaye sauti yake iliitetemesha nchi wakati ule; lakini sasa ameahidi akisema, Mara moja tena nitatetemesha si nchi tu, bali na mbingu pia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo