Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
Mika 1:15 - Swahili Revised Union Version Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki; Utukufu wa Israeli utafika Adulamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu. Biblia Habari Njema - BHND Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Enyi wakazi wa Maresha, Mungu atawaleteeni tena adui atakayewateka. Viongozi waheshimiwa wa Israeli watakimbilia pangoni huko Adulamu. Neno: Bibilia Takatifu Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu. Neno: Maandiko Matakatifu Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu. BIBLIA KISWAHILI Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki; Utukufu wa Israeli utafika Adulamu. |
Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?
Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko.