Methali 9:4 - Swahili Revised Union Version Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: Biblia Habari Njema - BHND “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!” Na yeyote aliye mpumbavu humwambia: Neno: Bibilia Takatifu Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! Neno: Maandiko Matakatifu Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa! BIBLIA KISWAHILI Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, |
Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.