Methali 9:3 - Swahili Revised Union Version Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko: Biblia Habari Njema - BHND Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amewatuma watumishi wake wa kike mjini, waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko: Neno: Bibilia Takatifu Amewatuma wajakazi wake, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. Neno: Maandiko Matakatifu Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji. BIBLIA KISWAHILI Amewatuma wajakazi wake, analia, Mahali pa mjini palipoinuka sana, |
Na kwa sababu hiyo hekima ya Mungu ilisema, Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na kuwafukuza,
akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njooni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri.
Katika siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!