Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwatawala watu wako hawa walio wengi?
Methali 4:7 - Swahili Revised Union Version Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili. Biblia Habari Njema - BHND Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili. Neno: Bibilia Takatifu Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu. |
Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwatawala watu wako hawa walio wengi?
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hatanyang'anywa.
Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;