Methali 4:17 - Swahili Revised Union Version Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya ujeuri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana uovu ndicho chakula chao, ukatili ndiyo divai yao. Biblia Habari Njema - BHND Maana uovu ndicho chakula chao, ukatili ndiyo divai yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana uovu ndicho chakula chao, ukatili ndiyo divai yao. Neno: Bibilia Takatifu Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri. Neno: Maandiko Matakatifu Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri. BIBLIA KISWAHILI Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya ujeuri. |
Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huku na huko na kusingizia.
BWANA asema hivi kuhusu manabii wanaowakosesha watu wangu; hao waumao kwa meno yao, na kulia, Amani; na mtu awaye yote asiyetia kitu vinywani mwao, wao humwandalia vita.
Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao.
Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.