Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Methali 31:5 - Swahili Revised Union Version Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Biblia Habari Njema - BHND Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Neno: Bibilia Takatifu wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote waliodhulumiwa. Neno: Maandiko Matakatifu wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa. BIBLIA KISWAHILI Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. |
Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.