Methali 3:34 - Swahili Revised Union Version Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Biblia Habari Njema - BHND Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Neno: Bibilia Takatifu Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu na walioonewa. Neno: Maandiko Matakatifu Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. BIBLIA KISWAHILI Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. |
Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.