Methali 3:21 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, zingatia hekima safi na busara; usiviache vitoweke machoni pako, Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara. |
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.
Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.