Methali 29:8 - Swahili Revised Union Version Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu. Biblia Habari Njema - BHND Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu. Neno: Bibilia Takatifu Wanaodhihaki huuchochea mji, bali wenye hekima huzuia hasira. Neno: Maandiko Matakatifu Wenye mzaha huuchochea mji, bali watu wenye hekima hugeuzia mbali hasira. BIBLIA KISWAHILI Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu. |
Ndipo BWANA akaniambia, Hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.
Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu.