Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Methali 29:13 - Swahili Revised Union Version Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili: Mwenyezi Mungu hutia nuru macho yao wote wawili. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: bwana hutia nuru macho yao wote wawili. BIBLIA KISWAHILI Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. |
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.