Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Methali 29:10 - Swahili Revised Union Version Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Biblia Habari Njema - BHND Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Neno: Bibilia Takatifu Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu. BIBLIA KISWAHILI Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. |
Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza BWANA kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema, ila mabaya. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.
Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza ya BWANA; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema kamwe, ila siku zote mabaya; naye ndiye Mikaya mwana wa Imla. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivyo.
Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.
Basi wakamwinua Yeremia kwa kamba hizo, wakamtoa shimoni; naye Yeremia akakaa katika ukumbi wa walinzi.
Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kwamba wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini;
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Si kwamba ninaupokea ushuhuda wa wanadamu; lakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.
Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha.