Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
Methali 27:6 - Swahili Revised Union Version Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli; Bali busu la adui ni udanganyifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu, lakini busu la adui ni udanganyifu. Biblia Habari Njema - BHND Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu, lakini busu la adui ni udanganyifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu, lakini busu la adui ni udanganyifu. Neno: Bibilia Takatifu Majeraha kutoka kwa rafiki yaonesha uaminifu, lakini adui huzidisha busu. Neno: Maandiko Matakatifu Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana. BIBLIA KISWAHILI Jeraha utiwazo na rafiki ni amani; Bali busu la adui ni udanganyifu. |
Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.