Methali 27:1 - Swahili Revised Union Version Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usijisifie ya kesho, hujui nini kitatokea leo mpaka kesho. Biblia Habari Njema - BHND Usijisifie ya kesho, hujui nini kitatokea leo mpaka kesho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usijisifie ya kesho, hujui nini kitatokea leo mpaka kesho. Neno: Bibilia Takatifu Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. Neno: Maandiko Matakatifu Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja. BIBLIA KISWAHILI Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. |
Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu yeyote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme.
Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Husema, Njooni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.
(Kwa maana asema, Kwa wakati uliokubalika nilikusikia, Na katika siku ya wokovu nilikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)
Tena pamoja na wewe BWANA atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena BWANA atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.