Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
Methali 26:26 - Swahili Revised Union Version Ingawa chuki hufunikwa na hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote. Biblia Habari Njema - BHND Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote. Neno: Bibilia Takatifu Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. Neno: Maandiko Matakatifu Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. BIBLIA KISWAHILI Ingawa chuki hufunikwa na hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. |
Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.
Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi.
Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya BWANA. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake.
Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu.