Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 26:27 - Swahili Revised Union Version

27 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe; abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe; abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe; abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake; mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

27 Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Tazama sura Nakili




Methali 26:27
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.


bali mfalme alipoarifiwa, aliamuru kwa barua ya kwamba huo mpango mwovu alioufanya juu ya Wayahudi umrudie kichwani pake mwenyewe; na ya kwamba yeye na wanawe watundikwe juu ya mti.


Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.


Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!


Mataifa wamezama katika shimo walilolichimba; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.


Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.


Maovu yake yeye yatampata mdhalimu, Naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake.


Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.


Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.


Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo