Sanbalati na Geshemu wakatuma wajumbe kwangu, wakasema, Njoo, tukutane huko vijijini katika nchi tambarare ya Ono. Lakini wakakusudia kunifanyia mabaya.
Methali 26:25 - Swahili Revised Union Version Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Biblia Habari Njema - BHND Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Neno: Bibilia Takatifu Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. Neno: Maandiko Matakatifu Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. BIBLIA KISWAHILI Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. |
Sanbalati na Geshemu wakatuma wajumbe kwangu, wakasema, Njoo, tukutane huko vijijini katika nchi tambarare ya Ono. Lakini wakakusudia kunifanyia mabaya.
Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha.
Kwa maana hata ndugu zako, na nyumba ya baba yako, wamekutenda mambo ya hila; naam, wamepiga kelele nyuma yako; usiwasadiki, wajapokuambia maneno mazuri.
Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.
Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya BWANA. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake.