Methali 23:20 - Swahili Revised Union Version Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, Biblia Habari Njema - BHND Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, Neno: Bibilia Takatifu Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, Neno: Maandiko Matakatifu Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, BIBLIA KISWAHILI Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. |
Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.
na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng'ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa.
Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
Na baada ya siku zisizokuwa nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Basi, jihadharini, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo;
Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi.