na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme.
Methali 22:11 - Swahili Revised Union Version Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye nia safi na maneno mazuri, atakuwa rafiki wa mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema, mfalme atakuwa rafiki yake. BIBLIA KISWAHILI Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. |
na Azaria mwana wa Nathani alikuwa afisa mkuu tawala; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki yake mfalme.
Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila.
Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?